Mwanasiasa mkongwe Mch Christopher Mtikila afariki dunia Leo asubuhi kwa ajali ya gari kwa taarifa zaidi bofya hapa @http.//too.gl/xDDNI2
Mwanasiasa mashuhuri nchini na Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party
(DP), Mch.Christopher Mtikila amefariki dunia na watu wengine watatu
kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Msolwa
kilichopo Chalinze mkoani Pwani alfajiri ya leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema Mtikila
amefariki majira ya saa 11:45 alfajiri ya leo katika kijiji cha Msolwa,
Chalinze.
Amesema gari alilokuwa amepanda Mtikila lilikuwa linatoka mkoani
Morogoro kwenda Dar es Salaam, ndani ya gari hilo kulikuwa na watu wanne
ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya na kupelekwa katika Hospitali
ya Tumbi iliyopo Kibaha, Pwani kwa matibabu.
Kwa habari zaidi endelea kufuatilia habari zetu tutakujuza hivi punde.
0 comments:
Post a Comment