Msemaji wa Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Mboza Luandiko akionyesha kwa
waandishi wa habari namba inayotumika katika kuhakiki taarifa za umiliki wa
viwanja na mashamba kwa kutumia simu ya mkononi kushoto ni Kamishna Msaidizi
Kanda ya Dar es salaam Bw. Mathew Nhonge.
Msemaji wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Bi Mboza Luandiko akifafanua kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani)
kuhusu namna mfumo mpya wa kuhakiki taarifa za umiliki wa viwanja na mashamba
kwa kutumia simu za mkononi utakakavyofanya kazi na kusaidia kupunguza kwa
kiasi kikubwa migogoro ya ardhi hapa nchini,kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi
wa TEHAMA Bw.Alexander Karaba.
Kamishna
Msaidizi Kanda ya Dar es salaam Bw. Mathew Nhonge akiwaeleza waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam kuwa Lengo la
Serikali ni kuhakikisha kuwa kila kipande cha Ardhi kinapimwa ili kuondoa
migogoro ya ardhi hapa nchini.
-----
Frank
Mvungi
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Msemaji wa Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Bi Mboza Luandiko wakati wa mkutano na waandishi wa habari
uliolenga kutambulisha huduma hiyo mpya kwa wananchi.
“Mfumo
huu unamwezesha mmiliki wa ardhi kuhakiki na kuboresha taarifa zake za ardhi
kwa kutumia simu yake ya mkononi kwa kuandika neno Ardhi kwenda namba 15774”
alisisitiza Luandiko
Akifafanua
Luandiko amesema kuwa wakati mwananchi anatuma ujumbe huo anatakiwa awea na
nyaraka zake za umiliki wa ardhi au barua ya toleo kwa wale ambao bado
hawajapata hati.
Akizungumzia
faida za mfumo huo Luandiko amebaini sha kuwa utasaidia kulinda milki za wateja
na kuondoa kabisa tatizo la matapeli.
Faida
nyingine ni kuongeza uwazi katika kugawa ardhi na hivyo kupunguza migogoro ya
ardhi ambapo hati milki zitatolewa kwa wingi zaidi kwa kuwa mfumo huo ni rafiki
katika utoaji wa huduma.
Aidha
mfumo huu utarahisisha Mawasiliano kati ya mmiliki wa ardhi na Wizara hali
itakayoongeza tija katika upatikanaji wa huduma kwa kuwa zinaweza kupatikana
kwa njia ya simu ya mkononi ikilinganishwa na hapo awali ambapo mwananchi
alitakiwa kufika katika Ofisi za Wizara ili kupata huduma husika.
Huduma ya
mfumo wa uhakiki wa taarifa za umiliki wa viwanja na mashamba imeanza katika
mkoa wa Dar es salaam na baada ya hapo tathmini itafanyika kabla ya kuanza
kutumika katika Mikoa yote.
0 comments:
Post a Comment