Top Ad 728x90

Thursday, October 29, 2015

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha ametangaza kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi zanzibar


Mwenyekiti wa ZEC,  Jecha Salum Jecha 
---
Tume ya Uchaguzi Zanzibar leo imetangaza kufuta uchaguzi na matokeo yake kwa kile ilichosema ni kuwa uchaguzi huo umegubikwa na ukiukwaji na taratibu za sheria za uchaguzi. Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha ametoa tangazo hilo leo kupitia televisheni ya taifa ya Zanzibar (ZBC). 

 
Akiongea baada ya kutolewa tangazo hilo, Katibu Mkuu wa CUF na ambaye alikuwa mgombea wa kiti cha urais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema hatambui uamuzi huo kwani mwenyekiti wa tume hana mamlaka ya kuamua bila kuwashirikisha makamishina.




Maalif Seif amesema wanawasiliana na taasisi za kimataifa na msaada juu ya jambo hilo.
 
Pia baada ya kutolewa kwa uamuzi huo na ZEC, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wamekutana na waandishi wa habari na kusema kuwa hawatakubali matokeo yanayoendelea kutolewa na NEC.

 
Hata hivyo, CCM kupitia Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za chama hicho, January Makamba amesema ni vema wanasiasa wakawana utaratibu wa kupokea na kukubali matokeo na kwamba anashangazwa na Ukawa kuanza kuonesha dalili za kuyakataa matokeo.

 
Akitolea ufafanuzi kuhusu uamuzi huo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema hilo halitaadhiri uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Muungano.Kwa maelezo zaidi bofya hapa http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/10/151028_zanzibar

0 comments:

Top Ad 728x90