Top Ad 728x90

More Stories

Sunday, October 1, 2017

KONGAMANO LA KUBWA LA KINABII NA UPONYAJI KUFANYIKA MOSHI,KILIMANJARO- P...

by

Sunday, March 27, 2016

SERIKALI YA TANZANIA HAINA MPANGO KWA KUTEKETEZA MENO YA TEMBO YALIYOHIFADHIWA

by

Serikali ya Tanzania imetoa tamko kuwa kwa sasa haina mpango wowote wa kuteketeza meno ya tembo yaliyohifadhiwa ambayo yametokana na vitendo vya ujangili na vifo asilia vya tembo.
Tamko hilo limetolewa hivi karibuni na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Mark Childress alipotembelewa na balozi huyo ofisini kwake kujadili maendeleo ya sekta ya Maliasili mchini.
Prof. Maghembe alisema hayo baada Balozi huyo wa Marekani hapa nchini kutoa pendekezo kwa Serikali ya Tanzania kuchoma sehemu meno ya tembo yaliyohifadhiwa ili kutoa ujumbe mzito duniani juu ya dhamira ya Serikali kukomesha biashara hiyo haramu.
"Naomba niweke wazi kuwa kwa sasa hatupo tayari kuteketeza meno haya, tunaweza kuyatumia kwenye tafiti za kisayansi au vielelezo kwa ajili ya kesi za ujangili ambazo zipo mahakamani na nyingine ambazo bado zinafanyiwa uchunguzi" Alisema Prof. Maghembe.
Zipo nchi mbalimbali duniani ambazo zimechukua hatua ya kuteketeza meno yake ya tembo yaliyohifadhiwa ikiwemo nchi jirani ya Kenya na Malawi ambapo inaaminika kuwa kufanya hivyo ni njia mojawapo ya kushawishi Ulimwengu kukomesha biashara hii haramu ya meno ya tembo.
Nchi nyingine ni Chad, Ubelgiji, Ufaransa, China, India, Marekani na Ureno. Kwa upande wa nchi ambazo zina msimamo sawa na Tanzania katika kuendelea kuhifadhi meno yake ya Tembo ni pamoja na Afrika ya Kusini, Botswana na Zimbabwe.
Akizungumzia kuhusu kuendeleza sekta ya Maliasili nchini, Prof.Maghembe amemuomba Balozi wa Marekani Bw. Mark Childress kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukuza sekta hiyo kwa kuleta wawekezaji mbalimbali kutoka Marekani kuja kuwekeza Tanzania pamoja na kusaidia kwenye mapambano dhidi ya Ujangili.
Aliongeza kuwa Tanzania ina fursa nyingi ambazo zinahitaji uwekezaji mkubwa ikiwemo hoteli za kitalii, fukwe za kisasa na kuendeleza vivutio mbalimbali vilivyomo hapa nchini.
Prof. Maghembe amemshukuru balozi huyo kwa misaada mbalimbali kutoka Serikali ya Marekani ya kuendeleza sekta ya Maliasili nchini ukiwemo wa hivi karibuni wa mbwa maalum (Snifer Dogs) kwa ajili ya kusaidia utambuzi wa rasilimali za Maliasili zinazoweza kutoroshwa nje ya nchi kupitia bandari na viwanja vya ndege.
Katika taarifa iliyowasilishwa kwenye kikao baina ya Waziri wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Mark Childress imeonesha kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Serikali ya Marekani imetoa misaada mbalimbali ambayo jumla yake ni dola za kimarekani Milioni 41.35 katika kusaidia eneo la uhifadhi hapa nchini.


Akizungumzia mahusiano baina ya Tanzania na Marekani Balozi Mark Childress alimueleza Prof. maghembe kuwa Serikali ya Marekani itaendeleza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi hizi mbili ambapo pia ofisi yake ya ubalozi imeshatafuta wadau mbalimbali ambao wapo tayari kusaidia fedha, vifaa na mafunzo kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi na mapambano dhidi ya ujangili. (Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)

MAJAMBAZI YAUA NA KUJERUHI JIJINI MWANZA

by

Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, SACP Justus Mamugisha, akitoa taarifa kwa wanahabari.--Watu wawili wameuawa Jijini Mwanza kwa kupigwa risasi na Majambazi, huku Wengine saba wakijeruhiwa katika tukio la uvamizi wa duka lililokuwa likitoa huduma mbalimbali za kifedha.Habari Zaidi BONYEZA HAPA.http://binagimediagroup.blogspot.com/2016/03/watu-wawili-wauawa-na-majambazi-jijini.html

MBIO ZA MAGARI ZA VAISAKH RALLY 2016 ZINAFANYIKA JUMAPILI HII VIWANJA VYA KIA,KILIMANJARO

by

 Mratibu wa Mashindano ya Mbio za Magari ya Vaisakh Rally 2016 ,Faheem Alooakizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani ) kuhusu maandalizi ya Mbio za Vaisakh Rally 2016 zinazofanyika Jumapili hii katika viwanja vya KIA


 MBIO ZA MAGARI ZA VAISAKH RALLY 2016 ZINAFANYIKA JUMAPILI HII VIWANJA VYA KIA,KILIMANJARO

 Zawadi kwa washindi.

 Hari Singh Rally Team ni moja ya madereva walioingiza gari mpya aina ya Subaru za mwaka 2015 katika mashindano hayo.
 Jamil Khan ataongoza team Evolution katika mashindano hayo.



Magari hapo juu ni ya madereva wengine watakao shiriki mashindano haya

Wednesday, January 6, 2016

TUMIENI VYOMBO VYA KIMATAIFA KUITANGAZA TANZANIA - WAZIRI MAGHEMBE

by
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Profesa Jumanne Maghembe akizungumza na Menejimenti ya Bodi ya Utalii leo jijini Dar es salaam.
.Kamimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi akitoa taarifa ya masuala mbalimbali yahusuyo Bodi yake mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Profesa Jumanne Maghembe wakati wa mkutano na Menejimenti ya TTB leo. Kulia kwa Bi Devota ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi Agelina Madata
Wajumbe wa Menejimenti ya TTB wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Bw. Ramo Makani  (wa pili kulia katika meza kuu) leo  jijini Dar es salaam.
---
Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe (MB) ameitaka Bodi ya Utalii Tanzania- TTB kuendelea kutumia vyombo vya habari vya Kimataifa kama vile CNN, BBC n.k kuitangaza Tanzania kama eneo la Utalii duniani sambasamba na kuweka makala na matangazo ya utalii wetu katika majarida ya Kimataifa yanayoandika habari za Utalii na usafiri (Travel Magazine) ambayo ndiyo husomwa na watalii wengi duniani.


 “Kama kweli tunataka kupata watalii wengi zaidi pamoja na mambo mengine ni lazima tutumie vyombo vikubwa vya Kimataifa vinavyofikia watu wengi zaidi duniani” alisema na kuongeza kuwa pamoja na njia nyingine zinazotumiwa katika kuitangaza Tanzania kimataifa, mbinu hii ya kutumia vyombo vya habari yaweza kuwa na ufanisi mkubwa zaidi .




Waziri Maghembe ameyasema hayo leo alipotembelea Bodi ya Utalii Tanzania na kukutana na Menejimenti  ya TTB kwa lengo la kujitambulisha na kubadilishana mawazo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi katika utangazaji utalii ndani na nje ya nchi.


Akizungumzia kuhusu madeni makubwa yanayoikabili TTB,  Mh. Profesa Jumanne Maghembe ameahidi kuwa Wizara yake itachukua madeni yanayoikabili TTB na hasa yaliliyotokana na maelekezo ya Wizara ya kama yale yaliyotokana na kuitaka Bodi iingie mikataba ya kuweka matangazo katika ligi kuu ya Uingereza na klabu za mpira wa mguu na Sunderland Football Association pia ya nchini Uingereza. 


Amesema Wizara ni lazima ilipe madeni hayo ili kulinda taswira ya Bodi ya Utalii kwa wadau na kuiondolea Bodi mzigo wa kuhangaikia madeni hayo badala yake ijikite zaidi katika kutangaza utalii.Kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa utalii nchini Profesa Maghembe amebainisha kuwa pamoja na uwepo wa mashirika mbalimbali ya ndege yanayokuja hapa nchini lakini kuna haja kubwa Tanzania kuwa na shirika lake imara la ndege ambalo litasaidia sana kukuza utalii nchini kama ilivyo kwa nchi nyingine kama Kenya na Afrka ya Kusini. 


Aidha amesema kuna haja pia ya kuboresha na kuendeleza zaidi  vivutio vyetu vya utalii na mazao mengine ya utalii kama vile Utalii wa fukwe na  Utalii wa utamaduni sambasamba na kukamilisha zoezi la uwekaji madaraja hoteli zetu na kutoa elimu kwa wenye hoteli kuboresha zaidi hoteli zao na hudiuma watoazo.


Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na viongozi wengine kutoka Wizarani akiwemo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Bw. Ramo Makani, Naibu katibu Mkuu Bi Angelina Madata na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Bw. Zahoro, Waziri Maghembe amesema anataka kuona idadi ya watalii ikiongezeka kutoka 1,100,000 ya sasa na kufikia Milioni 3,000,000  mwaka 2018.


Mapema kabla ya kumkaribisha waziri kuzungumza na Menejimenti, Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Bi Devota Mdachi alimwelezea Mh. Waziri mafanikio kadhaa ambayo Bodi imeyapata ikiwa ni pamoja na kuanzisha onesho la Utalii la Kimataifa la Swahili Swahili International Tourism Expo (S!TE) linalofanyika kila mwaka jijini Dar es salaam, kuanzishwa kwa tovuti maalumu (Portal) ya kuitangaza Tanzania na kulipia huduma nyingine za utalii moja kwa moja , uwekaji wa matangazo sehemu mbalimbali duniani.  


Bi Devota alimfahamisha pia Mh. Waziri kuwa TTB imechaguliwa kuwa miongoni mwa Bodi za Utalii tatu bora barani Afrika ambazo zinashindanishwa kumpata mshindi wa kwanza na wa pili. “Mh. Waziri, pamoja na matatizo mengi yanayoikabili TTB lakini tunafurahi kukujulisha kuwa TTB ni miongoni mwa bodi za utalii tatu zilizoingia katika hatua ya mwisho ya kutafuta mshindi wa Bodi ya Utalii borani Afrika tukishindana na Bodi za utalii za Afrika ya Kusini na Namibia katika shindano linaoendeshwa na taasisi ya Travvy ya Marekani” alidokeza Bi Mdachi.


Kaimu Mkurugenzi  huyo alidokeza pia kuhusu changamoto kadhaa zinazoikabili Bodi kubwa zaidi ikiwa ni madeni makubwa ya nje na ndani, na bajeti ndogo ya utangazaji.


Serikali yaanza kutumia mfumo wa simu za mkononi kuwawezesha wamiliki wa ardhi kuhakiki na kuboresha taarifa zao za ardhi kote nchini.

by
Msemaji wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Mboza Luandiko  akionyesha kwa waandishi wa habari namba inayotumika katika kuhakiki taarifa za umiliki wa viwanja na mashamba kwa kutumia simu ya mkononi kushoto ni Kamishna Msaidizi Kanda ya Dar es salaam Bw. Mathew Nhonge.
Msemaji wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Mboza Luandiko akifafanua kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu namna mfumo mpya wa kuhakiki taarifa za umiliki wa viwanja na mashamba kwa kutumia simu za mkononi utakakavyofanya kazi na kusaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya ardhi hapa nchini,kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TEHAMA Bw.Alexander Karaba.
Kamishna Msaidizi Kanda ya Dar es salaam Bw. Mathew Nhonge akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuwa Lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa kila kipande cha Ardhi kinapimwa ili kuondoa migogoro ya ardhi hapa nchini.
-----
Frank Mvungi



Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Msemaji wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Mboza Luandiko wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutambulisha huduma hiyo mpya kwa wananchi.

“Mfumo huu unamwezesha mmiliki wa ardhi kuhakiki na kuboresha taarifa zake za ardhi kwa kutumia simu yake ya mkononi kwa kuandika neno Ardhi kwenda namba 15774” alisisitiza Luandiko

Akifafanua Luandiko amesema kuwa wakati mwananchi anatuma ujumbe huo anatakiwa awea na nyaraka zake za umiliki wa ardhi au barua ya toleo kwa wale ambao bado hawajapata hati.

Akizungumzia faida za mfumo huo Luandiko amebaini sha kuwa utasaidia kulinda milki za wateja na kuondoa kabisa tatizo la matapeli.

Faida nyingine ni kuongeza uwazi katika kugawa ardhi na hivyo kupunguza migogoro ya ardhi ambapo hati milki zitatolewa kwa wingi zaidi kwa kuwa mfumo huo ni rafiki katika utoaji wa huduma.

Aidha mfumo huu utarahisisha Mawasiliano kati ya mmiliki wa ardhi na Wizara hali itakayoongeza tija katika upatikanaji wa huduma kwa kuwa zinaweza kupatikana kwa njia ya simu ya mkononi ikilinganishwa na hapo awali ambapo mwananchi alitakiwa kufika katika Ofisi za Wizara ili kupata huduma husika.

Huduma ya mfumo wa uhakiki wa taarifa za umiliki wa viwanja na mashamba imeanza katika mkoa wa Dar es salaam na baada ya hapo tathmini itafanyika kabla ya kuanza kutumika katika Mikoa yote.


ICHA NA TAARIFA KUTOKA IKULU: RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

by
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam.Picha na IKULU
----
http://3.bp.blogspot.com/-9GE3x5IfDJI/Vo1KpJCpTEI/AAAAAAADdbs/JGp-Qs2nLKo/s640/Kurugenzi%2Bya%2Bmawasiliano%2Bya%2BIkulu.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu Jijini Dar es salaam.


Katika Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Kikwete amemtakia Rais Magufuli heri ya Mwaka mpya na kumpongeza kwa uongozi mzuri.


Rais Kikwete pia amesema anaunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Rais Magufuli ikiwemo ukusanyaji wa mapato ya serikali.

WAZIRI MKUU KASSIMU MAJALIWA AMESEMA SERIKALI HAIJARIDHIA VIWANGO VIPYA VYA NAULI YA MABASI YAENDAYO KASI

by
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizunguza na Waandishi wa Habari kwenye uwanja wa Ngege wa Julius Nyerere baada ya kuwasili akitoka Songea Januari 6, 2016. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Geoge Simbachawene. na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es slaam Meck Sadiki
Baadhi ya waandishi wa habari wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere baada ya kuwasili akitoka Songea Januari 6, 2016. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu).PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu

---

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi vilivyopendekezwa na waendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo kasi Dar es salaam (UDART).
Akizungumza leo na waandishi wa habari, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku 3, Waziri Mkuu amesema Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi. Ambapo nauli ya kutoka Mbezi hadi Kimara shilingi 700, Mbezi hadi Kariakoo shilingi 1200, na nauli ya kutoka Mbezi hadi Mwenge shilingi 1400 na wanafunzi watatozwa nusu ya viwango hivyo vya nauli.
Waziri Mkuu amesema gharama hizi ni kubwa mno kwa wananchi na watumishi, mradi ulilenga kumrahisishia mtumishi wa Serikali anayeishi nje ya jiji, “Serikali iliwekeza katika mradi huu ili kusaidia watumishi na wananchi ambao hawana vipato vikubwa” alisema Waziri Mkuu.
Aidha, ameagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi, na Mawasiliano pamoja na wadau wakutane kupanga upya viwango hivyo na kama watashindwa basi Serikali itaendesha mradi huo.
Tarehe 25, Novemba 2015, Waziri Mkuu alimuagiza aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya TAMISEMI na waendeshaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi Dar es salaam (UDART) kupitia misuada yote na kurekebisha miundombinu ili mradi huo wa mabasi uanze kufanya kazi ifikapo tarehe 10, Januari 2016, imebainika kwamba UDART hawakuandaa mpango wa biashara wala kuanisha gharama za uendeshaji

Sunday, December 13, 2015

PICHA NA IKULU:RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

by
.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri,jana katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam














Rais Magufuli awaapisha Mawaziri na Manaibu

by
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akiapa mbele ya Rais John Magufuli
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amewaapisha Mawaziri na Manaibu waziri wapya Ikulu jijini Dar es salaam leo. Anaandika Faki Sosi … (endelea).
Jumla ya Mawaziri na Manaibu waziri 32 wameapishwa huku hatima ya wizara zingine nne ikiwa bado haieleweki kitendawili chake kitatenguliwa lini.
Wizara ambazo bado hatima yake iko gizani ni Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi,Wizara ya Maliasili na Utalii,na Wizara ya Fedha na Mipango, Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano.
Baraza hilo jipya lina sura mpya zipatazo 17 huku baadhi ya wakongwe walio hudumu katika awamu iliyopita wakizua maswali miongoni mwa jamii.
Baadhi ya Mawaziri wanaotiliwa shaka ni wale ambao waliondolewa kwa kashfa katika serikali ya awamu iliyopita
Habari zaidi bofya http://mwanahalisionline.com/rais-magufuli-awaapisha-mawaziri-na-manaibu/

Sumaye atangaza rasmi kuwa mwanachama wa Chadema

by
Waziri  mkuu wa awamu ya tatu Mh.Fredirick Sumaye ametangaza  rasmi kujiunga na chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema na  amekabidhiwa kadi na Mwenyekiti  wa chama hicho Mh.Freeman  Mbowe.
Sumaye ambaye wakati wa uchaguzi alitangaza kujiondoa  CCM na  kudai  kuwa  anaunga mkono  mageuzi yanayofanywa na vyama  vinavyounda  katiba  ya  wananchi (UKAWA) bila  kuweka  wazi  kuwa yuko kwenye chama kipi  kati ya  hivyo amesema asa ameamua  kujiunga na CHADEMA.

Akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni za ubunge wa  jimbo la Arusha  kwa chama cha CHADEMA uliofanyika kata ya baraa Sumaye  amesema anataka  kuungana na wanamageuzi wenzake katika  kuendeleza  harakati za mabadiliko hapa nchini ambazo bado  zinaendelea.

Akizungumza  baada ya kumkabidhi kadi Mwenyekiti wa chama hicho  Mh.Freeman Mbowe amesema chadema na vyama washirika wa  UKAWA bado viko imara na vimeendelea kuimarika na kwamba licha ya kudhulumiwa ushindi  azma yaoya  kuleta ukombozi  nchini iko  pale pale.


Awali aliyekuwa  mgombea urasi wa CHADEMA akiwakilisha vyama vya umoja wa katiba ya wananchi ukawa Mh.Edward Lowassa ameendelea kuwataka watanzania wanaounga mkono mabadiliko kuwa watulivu na kwamba kwa vile wana dhamira ya dhati ya kuyaona mabadiliko hakuna kukata tamaa kwani bado kuna fursa yakufikiwa  kwa malengo yao 

Friday, December 11, 2015

SOMA MAJINA YA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LILOTANGAZWA NA RAIS DR JOHN MAGUFULI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

by

BARAZA LA MAWAZIRI

Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri - George Simbachakene  na Angella Kairuki
Naibu Waziri - Sumeilam Jafo. Naibu.

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira
Waziri - January Makamba
Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri - Jenista Muhagama
MaNaibu – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri - Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri - William Ole Nasha

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani

Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri - Ashantu Kizachi

Wizara ya Nishati na Madini
Waziri - Prof. Mwigalumi Muhongo.
Naibu Waziri - Medalled Karemaligo.

Wizara ya Katiba na Sheria,
Waziri - Harrison Mwakyembe

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri - Dk. Augustino Mahiga
Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri - Dk. Hussein Mwinyi

Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri - Charles Kitwanga.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri - William Lukuvi
Naibu Waziri - Angelina Mabula

Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Charles Mwijage.

Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi.
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri - Ummy Mwalim
Naibu Waziri –  Dkt. Hamis Kigwangala

Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri - Nape Nnauye
Naibu Waziri - Anastasia Wambura.

Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Prof. Makame Mbarawa
Naibu  Waziri– Inj. Isack Kamwela


Wednesday, December 9, 2015

Raisi John Magufuli aongoza Watanzania kufanya usafi

by
Raia nchini Tanzania wameungana na maafisa wa serikali kuitikia wito wa Rais John Magufuli wa kutumia Siku ya Uhuru kufanya usafi.
Mamia ya watu walirauka na kuanza kusafisha baadhi ya maeneo ambayo hujulikana sana kwa kuwa na uchafu na taka kwa wingi.
Mwandishi wa BBC Sammy Awami aliwapata wachuuzi na maafisa wa baraza la jiji Dar es Salaam asubuhi na mapema wakifanya usafi katika soko maarufu la Kariakoo.
Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pia amefika soko hilo la Kariakoo.
Rais John Magufuli naye amekuwa kwenye aneo la ufuo wa bahari karibu na ikulu akiwa amevalia glavu.
Katika eneo la Mwenge, wananchi pia wanajizatiti kufanya usafi. Mwandishi wa BBC Regina Mziwanda amewapata wananchi hawa wakiteketeza takataka baada ya kuzikusanya pamoja.
Hata katika maeneo ya kifahari, wananchi wamejitokeza kufanya usafi.
Alipokuwa akitangaza kubadilishwa kwa utaratibu wa kusherehekea Siku ya Uhuru mwaka huu, Rais Magufuli alisema hatua hiyo italiokolea taifa pesa nyingi ambazo hutumiwa katika maandalizi na kufanikisha sherehe hizo.
“Fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua,” alisema.
Hata hivyo aliongeza kuwa sherehe hizo zitaendelea kuadhimisha kila mwaka kama kawaida kuanzia mwaka ujao.
Sikukuu hiyo huadhimishwa kila Desemba 9.

Top Ad 728x90

Top Ad 728x90