Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizunguza na Waandishi wa Habari kwenye uwanja wa Ngege
wa Julius Nyerere baada ya kuwasili akitoka Songea Januari 6, 2016. Kushoto ni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
Geoge Simbachawene. na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es slaam Meck Sadiki
Baadhi ya waandishi wa habari wananchi wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere baada ya
kuwasili akitoka Songea Januari 6, 2016. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu).PIcha
na Ofisi ya Waziri Mkuu
---
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haijaridhia
viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi vilivyopendekezwa na
waendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo kasi Dar es salaam (UDART).
Akizungumza leo na waandishi wa habari, mara baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini
Dar es salaam akitokea mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku 3, Waziri Mkuu amesema
Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi. Ambapo
nauli ya kutoka Mbezi hadi Kimara shilingi 700, Mbezi hadi Kariakoo shilingi
1200, na nauli ya kutoka Mbezi hadi Mwenge shilingi 1400 na wanafunzi watatozwa
nusu ya viwango hivyo vya nauli.
Waziri Mkuu amesema gharama hizi ni kubwa mno kwa wananchi
na watumishi, mradi ulilenga kumrahisishia mtumishi wa Serikali anayeishi nje
ya jiji, “Serikali iliwekeza katika mradi huu ili kusaidia watumishi na
wananchi ambao hawana vipato vikubwa” alisema Waziri Mkuu.
Aidha, ameagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene na
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi, na Mawasiliano pamoja na wadau wakutane kupanga
upya viwango hivyo na kama watashindwa basi Serikali itaendesha mradi huo.
Tarehe 25, Novemba 2015, Waziri Mkuu alimuagiza aliyekuwa
Katibu Mkuu Wizara ya TAMISEMI na waendeshaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi
Dar es salaam (UDART) kupitia misuada yote na kurekebisha miundombinu ili mradi
huo wa mabasi uanze kufanya kazi ifikapo tarehe 10, Januari 2016, imebainika
kwamba UDART hawakuandaa mpango wa biashara wala kuanisha gharama za uendeshaji
0 comments:
Post a Comment