Waziri mkuu wa
awamu ya tatu Mh.Fredirick Sumaye ametangaza rasmi kujiunga na chama cha
Demokrasia na maendeleo Chadema na amekabidhiwa kadi na Mwenyekiti
wa chama hicho Mh.Freeman Mbowe.
Sumaye ambaye wakati wa uchaguzi alitangaza
kujiondoa CCM na kudai kuwa anaunga mkono mageuzi
yanayofanywa na vyama vinavyounda katiba ya wananchi
(UKAWA) bila kuweka wazi kuwa yuko kwenye chama kipi
kati ya hivyo amesema asa ameamua kujiunga na CHADEMA.
Akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni
za ubunge wa jimbo la Arusha kwa chama cha CHADEMA uliofanyika kata
ya baraa Sumaye amesema anataka kuungana na wanamageuzi wenzake
katika kuendeleza harakati za mabadiliko hapa nchini ambazo bado
zinaendelea.
Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi
Mwenyekiti wa chama hicho Mh.Freeman Mbowe amesema chadema na vyama
washirika wa UKAWA bado viko imara na vimeendelea kuimarika na kwamba
licha ya kudhulumiwa ushindi azma yaoya kuleta ukombozi
nchini iko pale pale.
Awali aliyekuwa mgombea urasi wa CHADEMA
akiwakilisha vyama vya umoja wa katiba ya wananchi ukawa Mh.Edward Lowassa
ameendelea kuwataka watanzania wanaounga mkono mabadiliko kuwa watulivu na
kwamba kwa vile wana dhamira ya dhati ya kuyaona mabadiliko hakuna kukata tamaa
kwani bado kuna fursa yakufikiwa kwa malengo yao
0 comments:
Post a Comment