Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akitoa maelezo kuhusu idadi ya
wagonjwa waliopata huduma ya kipimo cha CT Scan baada ya mashine hiyo kukamilika
Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na
Televisheni nne ikipokelewa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH)
Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne
ikipokelewa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
---
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepata mashine
mpya na ya kisasa ya Digital X-ray ambayo wataalamu wake hawatalazimika kutumia
filamu kusafisha picha kama ilivyozoeleka katika mashine za kawaida.
Mashine hiyo imegharimu Dola 200,000 za Marekani ambazo
zimetolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo
ina uwezo wa kusafirisha picha nje ya nchi ili kupata ushauri wa kitaalamu.
Akilelezea kuhusu maendeleo ya mashine ya MRI na
CT-SCAN , Mkuu wa Idara ya Mionzi wa MNH, Dk Florah Lwakatare
amesema matengenezo ya mashine hizo yamekamilika na kwamba hadi sasa
wagonjwa 148 wamepimwa kwa kutumia mashine ya MRI , wakati wagonjwa 304
wamepimwa kwa kutumia CT-SCAN .
Katika hatua nyingine Hospitali ya Taifa Muhimbili leo
imepokea msaada wa mashuka 200, vyandarua 150 , Televisheni nne , Decoder
4 pamoja na Tv Stand 4.
Akikabidhi msaada huo ambao umetolewa na Kampuni ya Mr. Uk
Electronics Limited ya Dar essalaam, mwakilishi wa kampuni
hiyo John Solomon ametoa wito kwa jamii kuwa na
moyo wakujitolea na kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma mbalimbali
za jamii ikiwemo huduma za afya .
0 comments:
Post a Comment