Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), Hamis Chagonja
--By Peter
Elias, Mwananchi
Dar es Salaam. Zaidi ya
wanafunzi 52,000 wa mwaka wa kwanza watanufaika na mkopo wa elimu ya juu baada
ya Serikali kuongeza fedha kiasi cha Sh132 bilioni, kwa ajili ya kugharamia
masomo yao kwa mwaka wa masomo wa 2015/16.
Akizungumza na gazeti hili, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya
Elimu ya Juu (HESLB), Hamis Chagonja alisema bajeti ya Sh341 bilioni ilikuwa
imetengwa kwa ajili ya wanafunzi 14,226 wa mwaka wa kwanza.
Hata hivyo, alisema Serikali imeongeza fedha hizo hadi kufikia Sh473
bilioni ambazo zinatosha kuwalipa wanafunzi 52,000. Alisema ongezeko hilo
litawawezesha wanafunzi wengine 37,774 ambao hawakuwamo kwenye bajeti
kudhaminiwa na bodi yake kwa mwaka huu wa masomo.
“Kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao ni 71,125 hatuna shida sana,
wao wataweza kupata fedha hizo. Changamoto ilikuwa kwa hawa wa mwaka wa kwanza,
lakini sasa tumepata fedha za kuwalipa,” alisema
0 comments:
Post a Comment