Top Ad 728x90

Sunday, December 13, 2015

PICHA NA IKULU:RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

by
.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri,jana katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam














Rais Magufuli awaapisha Mawaziri na Manaibu

by
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akiapa mbele ya Rais John Magufuli
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amewaapisha Mawaziri na Manaibu waziri wapya Ikulu jijini Dar es salaam leo. Anaandika Faki Sosi … (endelea).
Jumla ya Mawaziri na Manaibu waziri 32 wameapishwa huku hatima ya wizara zingine nne ikiwa bado haieleweki kitendawili chake kitatenguliwa lini.
Wizara ambazo bado hatima yake iko gizani ni Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi,Wizara ya Maliasili na Utalii,na Wizara ya Fedha na Mipango, Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano.
Baraza hilo jipya lina sura mpya zipatazo 17 huku baadhi ya wakongwe walio hudumu katika awamu iliyopita wakizua maswali miongoni mwa jamii.
Baadhi ya Mawaziri wanaotiliwa shaka ni wale ambao waliondolewa kwa kashfa katika serikali ya awamu iliyopita
Habari zaidi bofya http://mwanahalisionline.com/rais-magufuli-awaapisha-mawaziri-na-manaibu/

Sumaye atangaza rasmi kuwa mwanachama wa Chadema

by
Waziri  mkuu wa awamu ya tatu Mh.Fredirick Sumaye ametangaza  rasmi kujiunga na chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema na  amekabidhiwa kadi na Mwenyekiti  wa chama hicho Mh.Freeman  Mbowe.
Sumaye ambaye wakati wa uchaguzi alitangaza kujiondoa  CCM na  kudai  kuwa  anaunga mkono  mageuzi yanayofanywa na vyama  vinavyounda  katiba  ya  wananchi (UKAWA) bila  kuweka  wazi  kuwa yuko kwenye chama kipi  kati ya  hivyo amesema asa ameamua  kujiunga na CHADEMA.

Akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni za ubunge wa  jimbo la Arusha  kwa chama cha CHADEMA uliofanyika kata ya baraa Sumaye  amesema anataka  kuungana na wanamageuzi wenzake katika  kuendeleza  harakati za mabadiliko hapa nchini ambazo bado  zinaendelea.

Akizungumza  baada ya kumkabidhi kadi Mwenyekiti wa chama hicho  Mh.Freeman Mbowe amesema chadema na vyama washirika wa  UKAWA bado viko imara na vimeendelea kuimarika na kwamba licha ya kudhulumiwa ushindi  azma yaoya  kuleta ukombozi  nchini iko  pale pale.


Awali aliyekuwa  mgombea urasi wa CHADEMA akiwakilisha vyama vya umoja wa katiba ya wananchi ukawa Mh.Edward Lowassa ameendelea kuwataka watanzania wanaounga mkono mabadiliko kuwa watulivu na kwamba kwa vile wana dhamira ya dhati ya kuyaona mabadiliko hakuna kukata tamaa kwani bado kuna fursa yakufikiwa  kwa malengo yao 

Friday, December 11, 2015

SOMA MAJINA YA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LILOTANGAZWA NA RAIS DR JOHN MAGUFULI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

by

BARAZA LA MAWAZIRI

Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri - George Simbachakene  na Angella Kairuki
Naibu Waziri - Sumeilam Jafo. Naibu.

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira
Waziri - January Makamba
Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri - Jenista Muhagama
MaNaibu – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri - Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri - William Ole Nasha

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani

Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri - Ashantu Kizachi

Wizara ya Nishati na Madini
Waziri - Prof. Mwigalumi Muhongo.
Naibu Waziri - Medalled Karemaligo.

Wizara ya Katiba na Sheria,
Waziri - Harrison Mwakyembe

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri - Dk. Augustino Mahiga
Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri - Dk. Hussein Mwinyi

Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri - Charles Kitwanga.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri - William Lukuvi
Naibu Waziri - Angelina Mabula

Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Charles Mwijage.

Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi.
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri - Ummy Mwalim
Naibu Waziri –  Dkt. Hamis Kigwangala

Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri - Nape Nnauye
Naibu Waziri - Anastasia Wambura.

Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Prof. Makame Mbarawa
Naibu  Waziri– Inj. Isack Kamwela


Wednesday, December 9, 2015

Raisi John Magufuli aongoza Watanzania kufanya usafi

by
Raia nchini Tanzania wameungana na maafisa wa serikali kuitikia wito wa Rais John Magufuli wa kutumia Siku ya Uhuru kufanya usafi.
Mamia ya watu walirauka na kuanza kusafisha baadhi ya maeneo ambayo hujulikana sana kwa kuwa na uchafu na taka kwa wingi.
Mwandishi wa BBC Sammy Awami aliwapata wachuuzi na maafisa wa baraza la jiji Dar es Salaam asubuhi na mapema wakifanya usafi katika soko maarufu la Kariakoo.
Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pia amefika soko hilo la Kariakoo.
Rais John Magufuli naye amekuwa kwenye aneo la ufuo wa bahari karibu na ikulu akiwa amevalia glavu.
Katika eneo la Mwenge, wananchi pia wanajizatiti kufanya usafi. Mwandishi wa BBC Regina Mziwanda amewapata wananchi hawa wakiteketeza takataka baada ya kuzikusanya pamoja.
Hata katika maeneo ya kifahari, wananchi wamejitokeza kufanya usafi.
Alipokuwa akitangaza kubadilishwa kwa utaratibu wa kusherehekea Siku ya Uhuru mwaka huu, Rais Magufuli alisema hatua hiyo italiokolea taifa pesa nyingi ambazo hutumiwa katika maandalizi na kufanikisha sherehe hizo.
“Fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua,” alisema.
Hata hivyo aliongeza kuwa sherehe hizo zitaendelea kuadhimisha kila mwaka kama kawaida kuanzia mwaka ujao.
Sikukuu hiyo huadhimishwa kila Desemba 9.

Tuesday, December 8, 2015

Serikali yaiongeza Bodi ya Mikopo Sh132 bilioni

by
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), Hamis Chagonja 
 --By Peter Elias, Mwananchi
Dar es Salaam. Zaidi ya wanafunzi 52,000 wa mwaka wa kwanza watanufaika na mkopo wa elimu ya juu baada ya Serikali kuongeza fedha kiasi cha Sh132 bilioni, kwa ajili ya kugharamia masomo yao kwa mwaka wa masomo wa 2015/16.

Akizungumza na gazeti hili, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), Hamis Chagonja alisema bajeti ya Sh341 bilioni ilikuwa imetengwa kwa ajili ya wanafunzi 14,226 wa mwaka wa kwanza.

Hata hivyo, alisema Serikali imeongeza fedha hizo hadi kufikia Sh473 bilioni ambazo zinatosha kuwalipa wanafunzi 52,000. Alisema ongezeko hilo litawawezesha wanafunzi wengine 37,774 ambao hawakuwamo kwenye bajeti kudhaminiwa na bodi yake kwa mwaka huu wa masomo.

“Kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao ni 71,125 hatuna shida sana, wao wataweza kupata fedha hizo. Changamoto ilikuwa kwa hawa wa mwaka wa kwanza, lakini sasa tumepata fedha za kuwalipa,” alisema

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepata mashine mpya na ya kisasa ya Digital X-ray ambayo wataalamu wake hawatalazimika kutumia filamu kusafisha picha kama ilivyozoeleka katika mashine za kawaida

by
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu matumizi ya mashine mpya ya X-ray ya digitali.  Dk Lwakatare amesema mashine hiyo ina uwezo wa kupiga picha na kutumwa nje ya nchi kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu zaidi. Mashine hiyo haihitaji chumba cha kusafishia picha wala dawa za kusafisha
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akitoa maelezo kuhusu idadi ya wagonjwa waliopata huduma ya kipimo cha CT Scan baada ya mashine hiyo kukamilika
Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
---
Hospitali ya Taifa  Muhimbili (MNH) imepata mashine mpya na ya kisasa ya Digital X-ray ambayo wataalamu wake hawatalazimika kutumia filamu kusafisha picha kama ilivyozoeleka katika  mashine za kawaida.

Mashine hiyo imegharimu Dola 200,000 za Marekani ambazo zimetolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  ambayo ina uwezo wa kusafirisha picha nje ya nchi ili kupata ushauri wa kitaalamu.

Akilelezea kuhusu maendeleo ya mashine ya MRI na CT-SCAN  , Mkuu wa Idara ya Mionzi wa MNH,  Dk Florah  Lwakatare amesema matengenezo ya mashine hizo  yamekamilika na kwamba hadi sasa wagonjwa 148 wamepimwa  kwa kutumia mashine ya MRI , wakati wagonjwa 304 wamepimwa kwa kutumia CT-SCAN . 

Katika hatua nyingine Hospitali ya Taifa Muhimbili leo imepokea msaada wa mashuka 200, vyandarua 150 ,  Televisheni nne , Decoder 4 pamoja  na Tv Stand 4.

Akikabidhi msaada huo ambao umetolewa na Kampuni ya Mr. Uk Electronics Limited ya Dar essalaam, mwakilishi wa kampuni hiyo    John Solomon   ametoa wito kwa jamii kuwa na moyo wakujitolea na kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma mbalimbali za jamii ikiwemo  huduma za afya .

WIMBO MPYA WA MUDY WHITE -----MANENO...Track mudy+white

by

Msanii wa Kizazi kipya yani Bongo fleva Muddy White ametoa ngoma yake kali kabisa inayokwenda kwa Jina la Maneno. Amesema nyimbo hii ni moja tu kati ya nyimbo nyingi ambazo anatarajia kutoa na ambazo ameshatoa hivyo akiwaomba mashabiki wake wawe tulivu na wa subira kungojea Nyimbo nyingine kali 

posted by Baraka

Top Ad 728x90