Top Ad 728x90

Thursday, October 29, 2015

Lowassa apinga matokeo ya Uchaguzi yalitangazwa na NEC

by

Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA Edward Lowassa amesema kuwa hatokubali matokeo ya uchaguzi wa urais yanayoendelea kutolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC).
Kiongozi huyo amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha kwamba kuna udanganyifu uliofanyika.
Amesema kuwa kura za chama hicho zimepunguzwa katika vituo vingi vya kupigia kura.
Akihutubia wanahabari pamoja na viongozi wengine wa upinzani, amesema kwamba kura zilizohesabiwa katika maeneo tofauti haziambatani na matokeo yaliyotolewa.
Lowassa ameongezea kwamba maeneo yote ambayo walipata ushindi yamecheleweshwa. Aidha, amelalamikia kukamatwa kwa maajenti wa chama hicho akidai kuwa ni ishara za kutaka kuiba kura.

BREAKING NEWS: Mgombea urais wa chama cha CCM Mh. John Pombe Magufuli ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya tano

by

BREAKING NEWS: Mgombea urais wa chama cha CCM Mh. John Pombe Magufuli ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya tano kwa kupata kura milioni 8,882,935 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Edward Lowassa aliyepata kura milioni 6,072,848HONGERA SANA DK. JOHN POMBE MAGUFULI

Mama Samia Hassan Suluhu mgombea mwenza wa CCM anaweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Makamu wa Rais nchini Tanzania. Ametangawa rasmi na Tume ya uchaguzi kushinda kiti hicho cha Makamu wa Rais wa Tanzania

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YATANGAZA MHESHIMIWA DKT.JOHN POMBE MAGUFULI KUWA MSHINDI WA UCHAGUZI MKUU 2015 KWA 58.46%

by
Tume ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza matokeo ya Uraisi na kumtaja Mhe DrJohn Pombe Magufuli mgombea Uraisi kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi kuwa mshindi na Rais Mteule - Hivyo Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Damian Z. Lubuva
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumtangaza kuwa Mshindi kwa asilimia 58.46%
Huku Vyama vingine vya siasa kama chadema [37.97%] kwa maelezo zaidi tutaendelea kukujuza bofya hapa kufahamu zaidi http://www.hakingowi.com/2015/10/rais-ni-magufuli-tume-yamtangaza.html
MATOKEO

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha ametangaza kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi zanzibar

by

Mwenyekiti wa ZEC,  Jecha Salum Jecha 
---
Tume ya Uchaguzi Zanzibar leo imetangaza kufuta uchaguzi na matokeo yake kwa kile ilichosema ni kuwa uchaguzi huo umegubikwa na ukiukwaji na taratibu za sheria za uchaguzi. Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha ametoa tangazo hilo leo kupitia televisheni ya taifa ya Zanzibar (ZBC). 

 
Akiongea baada ya kutolewa tangazo hilo, Katibu Mkuu wa CUF na ambaye alikuwa mgombea wa kiti cha urais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema hatambui uamuzi huo kwani mwenyekiti wa tume hana mamlaka ya kuamua bila kuwashirikisha makamishina.




Maalif Seif amesema wanawasiliana na taasisi za kimataifa na msaada juu ya jambo hilo.
 
Pia baada ya kutolewa kwa uamuzi huo na ZEC, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wamekutana na waandishi wa habari na kusema kuwa hawatakubali matokeo yanayoendelea kutolewa na NEC.

 
Hata hivyo, CCM kupitia Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za chama hicho, January Makamba amesema ni vema wanasiasa wakawana utaratibu wa kupokea na kukubali matokeo na kwamba anashangazwa na Ukawa kuanza kuonesha dalili za kuyakataa matokeo.

 
Akitolea ufafanuzi kuhusu uamuzi huo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema hilo halitaadhiri uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Muungano.Kwa maelezo zaidi bofya hapa http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/10/151028_zanzibar

Friday, October 16, 2015

MH. DEOGRATIUS HAULE FILIKUNJOMBE AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA HELIKOPTA

by

Chopa aliyokuwa amepanda Mh.Deogratius HauleFilikunjombe iliyopata ajali maeneo ya mbuga ya selous


Waokoaji wakibeba mabaki ya mwili wa marehemu wa ajali hiyo ya Helikopta

Timu ya maofisa na askari wataalamu wakikagua mabaki ya chopa iliyoanguka sehemu ya wanyama selous iliyokuwa ikitokea Dar kuelekea Ludewa ambapo Mh.Captain Komba Rubani Capt Wiliam Slaa na abiria wengine wawili  waliopoteza maisha

Chanzo cha habari kinasema Mh.Filiponjombe na Rubani wake walipata matatizo ya Engine ya chopa waliokuwa wamepanda yenye namba 5Y-DDKNa kwa mujibu wa Meya wa Halmashauri ya Ilala aliyemaliza muda wake Jerry Slaa ambaye ni mtoto wa Marehemu amesema hakuna majeruhi katika ajali ya kwamba wote walikuwemo walipoteza maisha

Sunday, October 4, 2015

HAYA NDIO ALIYONGEA MWANASIASA MKONGWE MH.KINGUNGE WAKATI AKITANGAZA KUJIVUA CCM

by
* MWASISI WA TANU/CCM, MZEE KIGUNGE ATEMA CHECHE
* AJIVUA UANACHAMA WA CCM
* ASEMA CCM IMEBINAFSISHWA
Anasema kamati kuu haiwezi kusema watu watano au sita ni hawa bila kuwasikiliza, kilichotokea mwaka huu ni tofauti kabisa kilichotokea mwaka 1995, safari mwenyekiti ni Jakaya Kikwete, kilichotokea ni jambo kubwa katika historia yetu na mimi katika historia yangu pale ambapo naona kwamba katiba inavunjwa nimekuwa na tabia ya kusema waziwazi na kuwaambia wenzangu si sawa.
Mwaka 1972 nikiwa mkuu wa mkoa Simiyu, kulikuwa na Bunge Dar es Salaam, nikakuta kuna mswada wa kurekebisha katika kuhusiana na swala la wakuu wa mikoa. Mchango wangu uliibua hisia kali na kumwambia mwenyekiti muswada aurudishe maana hatuukubali, kwa upande wa watu walipo serikalini walisema ndio na wabunge wa kuchaguliwa walisema hapana.
Ilipofika zamu yangu nikasema sina upande, wabunge walifurahi sana. Kura zilipohesabiwa serikali ilishindwa kwa mara ya kwanza katika mfumo wa serikali ya chama kimoja. Mzee Kawawa aliniita akasema wewe ni mwenzetu lakini umetuacha, Rais atakubadilisha kazi.
Nilipoitwa na mwalimu nilimueleza kwa nini nilikataa na akasema ningekuwa katika nafasi yako ningepinga lakini mimi ndio naongoza nchi lakini usiwe na wasiwasi. Tukakubaliana na siku ya pili nikatangazwa nimeachishwa uwaziri. Nilifanya uamuzi ule nikijua kabisa naweza kupoteza kazi lakini kwenye masula ya kimsingi huwa sitetereki.
Mimi sikubaliani na mambo yaliyotokea tarehe kumi na kumi na moja Dodoma, kilichotokea ni kuwadhalilisha wagombea wenye haki, kamati kuu ingeweza kuwahoji na kuamua. Hili halikfanyika. wadhalilishwa, wamezungushwa mikoa 15 kwa gharama zao na kuishia mlangoni mwa kamati kuu.
CCM inaamini binadamu wote ni sawa na kila mtu anastahili heshma ya kutambuliwa utu wake, kuwazungusha alafu nyinyi mmefunga mlango, si kuwadhalilisha? Katika nchi yetu hao waliodhalilishwa wamenyamaza moja kwa moja isipokuwa Mwandosya, aliinuka na kusema kwamba kweli wamedhalilishwa na kadhalika.
Nawapongeza Kimbisa, Sophia na Nchimbi kwa kueleza yaliyotokea kamati kuu, tuliingia chama hiki si kwa ajili ya kutafuta cheo na wengine tuliacha kazi kwa mkoloni. Tulitafuta chombo cha ukombozi kwa watanzania na waafrika.
Kwa kuwa uongozi wa sasa wa chama cha mapinduzi kufanya yale wanayotaka wao kwa maslahi ambayo sina hakika ni ya nani, vijana wanatumiwa kudhalilisha watu wazima, watu wanaajiriwa kutukana tu watu, mimi nasema sikubaliani na hiko sio chama tulichoshirikiana kukijenga.
Mimi kuanzia leo naachana na chama cha mapinduzi kwa sababu siwezi kuhimili chama kinachoendeshwa bila kuheshimu katiba kwa sababu katiba ndio inayotuunganisha sisi sote. Sasa nasema kuanzia sasa najitoa chama cha mapinduzi, najua uamuzi wangu utasumbua baadhi ya rafiki zangu, makada wenzangu na wazee wenzangu hata vijana lakini ni uamuzi ambao lazima niufanye kwa sababu vinginevyo mimi nitajisaliti mwenyewe.
Nimehusika kuweka misingi ya chama chetu, ndani ya chama chetu kumekuwa na demokrasia halafu wakuu wanakwenda kutangaza kwenye majukwaa hakukuwa na tatizo lolote, mambo yote yalikuwa sawasawa.
Sikusudii kujiunga na chama kingine chochote na nina sababu, mimi nimekuwa mwanaharakati wa TANU na CCM kwa muda wa miaka 61, nadhani miaka 61 inatosha mimi kuwa mwanaharakati.
Tatu mimi ni raia tena raia huru wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, nna haki zangu za kisisasa na kijamii hivyo nitaendelea misimamo yangu.
Katika hali ya sasa ina makundi mawili, moja linasema kidumu chama tawala maana yake hakuna mabadiliko. Kundi jingine linasema linataka mabadiliko katika nchi yetu, sitaki kusema kundi lipi kubwa lakini nasema hali iko hivyo, kwa jinsi nnavyotazama vijana wanataka mabadiliko ukiondoa vijana wangu wa UVCCM, kina mama walio wengi wanataka mabadiliko, wafanyakazi wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimba migodi wadogowadogo najua wengi wao wanataka mabadiliko, wanafunzi hasa wa sekondari ya juu, wa vyuo na vyo vikuu na wasomi wa nchii walio wengi wanataka mabadiliko.
Nilisema siku moja nilipoulizwa nani unamuona anafaa kugombea Urais, niliwaambia kwamba mimi nitamuunga mkono yule ambae ziko dalili zote wananchi wanasema ndie anaefaa. Pia nilisema nilipokuwa na ndugu Lowassa Arusha, Mwalimu alisema ulizeni wananchi wanasema nini?
Katika hili swala la mabadiliko mimi niko upande wa mabadiliko tena mimi nasema wamechelewa, walio wengi wanataka mabadiliko. Mimi nasema niko upande wa mabadiliko kwa sababu ya wale. Katika historia yetu katika TANU na Afro shirazi sisi tulikuwa upande wa mabadiliko.
Tuliungana na hio ilikuwa mabadiliko, mwaka 77 tuliua Afro Shirazi, tuliua TANU na kufanya mabadiliko.
Baada ya kukaa madaraki miaka mingi hatuwezi kuleta jipya pamoja na ahadi za Magufuli, nusu karne ni muda mrefu sana, pumzi, kuongoza nchi na kama kupanda mlima, unafika mahala pumzi zinakwisha, huwezi kuendelea mbele na ukitaka kuendelea wananchi wanabaki palepale walipo.
Tatizo la wananchi ni uchumi, ajira, sasa umasikini unaondolewa na uchumi imara.
Mkapa alitufanyia kazi nzuri kwa kututoa kwenye ukuaji wa asilimia 3 mpaka 4, wakati anakabidhi madaraka ulikuwa unakuwa kwa 7%. Kikwete amepokea madaraka unakuwa kwa 7%, sasa miaka kumi baadae uchumi unakuwa kwa 7%. Maana yake miaka kumi hii tumepiga maktaimu, tumebaki palepale maana yake ni kurudi nyuma.
Idadi ya watu imeongezeka, midomo imeongeza, miguu imeongezeka lakini ukuaji uko palepale, bei ya sukari kwa mfano ni ya kuruka, bei ya sukari Mkapa aliacha 600 sasa inaenda 2000. Nini! Pumzi. Kwenda kwenye maisha bora kunataka pumzi.
Tulianza na maisha bora kwa kila mtanzania lakini sasa hatusemi tena habari hizo, mabadiliko ni muhimu kwelikweli, tupate pumzi mpya. Mnataka mbaki nyinyi tu, nyinyi pumzi imekwisha. Chama kifutike? Hapana lakini kiwekwe benchi kidogo kijitafakari.
Kama hamjadili mambo mtapata wapi mawazo ya kwenda mbele, lazima ukuaji wa uchumi wa nchi angalau ufike 10%. 7% mpaka 10% si mbali lakini miaka kumi tuko palepale. Wachina wamekuwa wakikuza uchumi wao mpaka asilimia 15 na zaidi, na sisi hapa baadhi yetu kama watu watakuwa wanyenyekevu kupata mawazo ya wenzao tutapiga hatua.
Mimi nimekuwa mwenyekiti wa ilani zote za uchaguzi kasoro moja tangu mwaka 90, tatizo la ajiri kwa vijana linaonekana kana kwamba halitatuliki wakati linatatulika, kujiajiri na kutoa mitaji. Wanaotaka kujidanganya kwamba wataleta mabadiliko haya!
Lakini tunaotaka kwenda mbele, kung'ang'ania kwamba lazima wao wawe madarakani mtakuja kujilaumu wenyewe siku moja. Asanteni sana kwa kunisikiliza.
SWALI(Mayage): Kama CCM mngemteua Lowassa, ungayasema hayo ya kusema unataka mabadiliko
Jibu: Mimi wakati wote nimekuwa nina matumaini kwamba ndani ya CCM tunaweza kupata watu wanaoweza kubadili hali ndio maana niliamua kupambana ndani ya chama changu tukaenda mbio kuliko hivi ili hali ya wananchi ibadilike. Mimi nikamuona Edward Lowassa kwa jinsi ninavyomjua, si mtu mgeni katika nchi hii, nikasema tukimpata nchi itakwenda mbio zaidi.
Niliwahi kuzungumza kwanini nilisimama sambamba na Edward Lowassa kule Arusha, nikasema Edward ana sifa kuliko wengi niliowaona, kiongozi lazima akubalike na watu na hii ni principle ya watu tangu TANU, Lowassa anakubalika pamoja kupakaziwa mambo ya ajabu.

HATIMAYE MWANASIASA NGULI MHESHIMIWA KINGUNGE AJITOA RASMI KATIKA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM

by

Kingunge ajitoa rasmi ccm leo Alipokataa kuunga mkono muswada aliitwa Siku ya pili akatangazwa ameachishwa ukuu."Kwenye masuala ya kimsingi mimi hua Sikubaliani na yaliyotokea Dodoma".Alisema Ni uvunjifu wa katiba, kuwadhalilisha wagombea waliokuwa na haki ya kufika kamati kuu na kuhojiwa na wajumbe Waliambiwa wazunguke mikoa kumi kutafuta wadhamini kwa gharama zao....wanakuja wanaishia mlangoni kwa kamati kuu!

Kingunge amesema hawezi kushirikia na Chama chenye Ubaguzi kisichoangalia nini wananchi wanataka na Kusema CCM haiwezi kuiletea tena Tanzania Maendeo kwa sasa na kuwaasa watanzania kufanya Mabadiliko yatakayowafikisha kwenye maendeleo katika Taifa letu

TAMASHA LA KULIOMBEA TAIFA AMANI JUMAPILI OCT 4 HUKU SOLLY MAHLANGU NA IFYEANYI WATUA KUKOLEZA UTAMU

by

Msanii wa Nyimbo za Injili kutokea Ulaya ifyeanyi katikati akiwasili leo katika uwanja wa Kimataifa wa Julias Nyerer tayari kushiriki katika Tamasha leo la kuliombea Taifa Amani.Kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama na kushoto ni mratibu Hudson kamoga 

Tamasha Hilo ambalo litahudhuriwa na maelfu Ya Watanzania huku Viongozi zaidi ya wachungaji 200 pamoja na maaskofu zaidi ya 50 kushiriki 

kwa habari zaidi bofya hapa @http://issamichuzi.blogspot.com/2015/10/jk-kuongoza-maelfu-kuombea-amani.html

chanzo cha habari Michuzi Blog

Saturday, October 3, 2015

MCHUNGAJI MTIKILA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI NA WENGINE WATATU KUJERUHIWA

by
Mwanasiasa mkongwe Mch Christopher Mtikila afariki dunia Leo asubuhi kwa ajali ya gari kwa taarifa zaidi bofya hapa @http.//too.gl/xDDNI2

Mwanasiasa mashuhuri nchini na Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party (DP), Mch.Christopher Mtikila amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Msolwa kilichopo Chalinze mkoani Pwani alfajiri ya leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema Mtikila amefariki majira ya saa 11:45 alfajiri ya leo katika kijiji cha Msolwa, Chalinze.

Amesema gari alilokuwa amepanda Mtikila lilikuwa linatoka mkoani Morogoro kwenda Dar es Salaam, ndani ya gari hilo kulikuwa na watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya na kupelekwa katika Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha, Pwani kwa matibabu.

Kwa habari zaidi endelea kufuatilia habari zetu tutakujuza hivi punde.

Top Ad 728x90