Top Ad 728x90

Monday, November 9, 2015

RAISI MHE.DKT JOHN POMBE MAGUFULI ATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI AKUTA HALI TETE

by

Raisi Magufuli akitembelea katika Hospitali kuona hali ilivyo ndani ya hospitali hiyo na kukutana na hali tete baada ya kuona wagonjwa wakilala chini kwa kukosa vitanda na wengine wakikosa matibabu na kufunja Uongozi wa Hospitali huo na kuchagua Bodi mpya ya Muda 

RAISI MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI, AVUNJA UONGOZI NA KUCHAGUA UONGOZI WA MUDA

by

 Rais Dk. John Pombe Magufuli amevamia tena leo katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili na kutembelea wagonjwa mbalimbali pamoja na kuzungumza nao, ili kujua matatizo wanayokabiliana nayo katika kupata huduma, Dk. Magufuli pia amemjulia hali Mkurugenzi wa Kituo cha  Sheria na  haki za binadamu LHRC Mama Hellen Kijo Bisimba ambaye amelazwa hospitalini hapo kutokana na majereaha aliyoyapata wakati alipopata ajali na gari lake maeneo ya Upanga jijini Dar es salaam na kulazwa hospitalini hapo



AKIWASALIMIA WAGONJWA MBALIMBALI KATIKA HOSPITALI


Rais Dk. John Pombe Magufuli Mkurugenzi wa Kituo Sheria na  haki za binadamu LHRC Mama Hellen Kijo Bisimba ambaye amelazwa hospitalini hapo kutokana na majereaha aliyoyapata wakati alipopata ajali na gari lake maeneo ya Upanga jijini Dar es salaam na kulazwa hospitalini hapo.

Saturday, November 7, 2015

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AONDOKA RASMI IKULU NA KUELEKEA KIJIJINI MSOGA LEO

by

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AONDOKA RASMI IKULU NA KUELEKEA KIJIJINI MSOGA LEO

 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati wakiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita na kurudi kijijini Msoga. kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Maguful
 Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete   wakati akiondoka rasmi Ikulu alimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita
 Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete   na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu alimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita.
 Wakielekea kwenye helikopta itayowachukua hadi kijijini Msoga
  Picha ya pamoja kabla safari ya Msoga kuanza
  Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiagana na  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete   na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu walimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita.
Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Katibu Mkuu Ikulu Mhe Peter Ilomo na watumishi wa Ofisi ya Rais wakiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho kikwete habari zaidi bofya @http://www.hakingowi.com/2015/11/rais-mstaafu-jakaya-kikwete-aondoka.html#more

MHUBIRI WA KIMATAIFA TB JOSHUA ALIPOKUTANA NA EDWARD LOWASSA NA VIONGOZI WA UKAWA

by

Mh. Edward Lowassa akimkaribisha mgeni wake, Muhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Nigeria, TB Joshua, wakati alipomtembelea kwa mara nyingine nyumbani kwake, Masaki Jijini Dar es Salaam juzi Novemba 4, 2015.

 Muhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Nigeria, TB Joshua, akizungumza jambo na Mh. Edward Lowassa pamoja na viongozi wakuu wa UKAWA, Mh.Freeman Mbowe, Mh. James Mbatia na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru.Picha na Othman Michuzi

Top Ad 728x90